Ni ipi hukumu ya kusindikiza jeneza la muislamu?

Swali: Ni ipi hukumu ya kusindikiza jeneza la muislamu? Ni wajibu kwa waislamu wote?

Jibu: Wanachuoni wanasema kumuosha maiti, kumvisha sanda, kumbeba na kumzika ni wajibu kwa baadhi ya waislamu. Kukipatikana wataofanya hayo hakuna haja ya wengine kufanya hivo. Lakini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekokoteza kushiriki katika kulisindikiza jeneza na kusema:

“Atayelishuhudia jeneza mpaka likaswaliwa, basi ana Qiraatw. Na yule atayelishuhudia mpaka likazikwa, ana Qiraatw mbili.” Kukasemwa: “Qiraatw mbili ni nini?” Akasema: “Ni mfano wa milima miwili mikubwa.”[1]

[1] al-Bukhaariy (1325) na Muslim (945).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/167-168)
  • Imechapishwa: 25/08/2021