Ni ipi hukumu ya kuliwekea jeneza kitambaa kilichodariziwa pindi anapowekwa ndani ya kaburi?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuliwekea jeneza kitambaa kilichodariziwa linapowekwa ndani ya kaburi? Muslim amepokea kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) aliyesema:

“Kuliwekwa kitambaa chekundu kilichodariziwa kwenye kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[1]

Jibu: Wanachuoni wamesema kuwa haina neno. Lakini mimi naonelea hili linatakiwa kuangaliwa. Kwa kuwa haikupokelewa kutoka kwa Swahabah yeyote ya kwamba alifanya hivo. Huenda ilikuwa ni jambo maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Nachelea ukifunguliwa mlango huu watu wakaanza kushindana juu ya hilo. Itakuwa kila mmoja anataka maiti wake awe na kitambaa kilichodariziwa kilicho bora kuliko mwengine. Hatimaye makaburi yageuke ni mahali pa matapo. Kila kinachopelekea katika makatazo kinatakiwa kuzuiwa.

[1] Muslim (967).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/183-184)
  • Imechapishwa: 25/08/2021