Ni ipi hukumu ya kuchimba kaburi pasi na mwanandani?

Swali: Baadhi ya watu ardhi yao ni ya mchanga na makaburi yao yanachimbwa moja kwa moja kwenda chini pasi na mwanandani. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ikiwa kuna haja ya kuchimba moja kwa moja kwenda chini hakuna neno. Bali inaweza kuwa wajibu, kama ilivyo katika ardhi za mchanga.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/178)
  • Imechapishwa: 25/08/2021