Ni ipi hukumu ya kuyachimbua makaburi kwa ajili ya kupitisha barabara?

Swali: Inajuzu kuyachimbua makaburi ili kujenga njia ya watu wote ikiwa hakuna namna ya kukata barabara isipokuwa kupitia makaburi? Inajuzu kuyachimbua na kuyaweka sehemu nyingine ya makaburi?

Jibu: al-Lajnah ad-Daaimah nchini Saudi Arabia, au baadhi ya wanachuoni wake, wametoa fatwa ya kwamba inajuzu kuyachimbua makaburi wakati wa dharurah kwa ajili ya kujenga barabara ikiwa hakuna namna nyingine. Makaburi yachimbuliwe kwa sharti mifupa ichukuliwe na kuhamishwa sehemu nyingine kwenye makaburi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/203)
  • Imechapishwa: 25/08/2021