Ni ipi hukumu ya kulifukua kaburi ili kuchukua dhahabu ya maiti?

Swali: Kuna msichana mmoja aliungua mahali kuliposhika moto mpaka akafa. Tulipokuwa tukimuosha na kumzika tukaona kuwa alikuwa na dhahabu mkononi mwake na mahereni. Inajuzu kulichimbua kaburi kwa ajili ya kuchukua ile dhahabu?

Jibu: Hakuhitajiki kuchimbua kaburi la msichana huyo kwa ajili ya kuchukua dhahabu aliokuwa nayo. Lakini wanaweza kufanya hivo ikiwa yamepitika katika kipindi cha karibu huko mbeleni baada ya mazishi. Dhahabu ni mali yao baada ya kufa kwa msichana huyo. Lakini iwe baada ya kurejea katika mamlaka husika ili mambo yasiwe ya vurugu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/203-204)
  • Imechapishwa: 25/08/2021