Ni ipi hukumu ya kupita na viatu kati ya makaburi?

Swali: Ni ipi hukumu ya kupita na viatu baina ya makaburi? Ni upi usahihi wa dalili inayokataza hilo:

“Ee uliye na viatu vya ngozi! Vua viatu vyako.”[1]?

Jibu: Wanachuoni wanasema kuwa kupita kati ya makaburi na viatu ni jambo limechukizwa. Wametumia dalili kwa Hadiyth hii. Lakini hata hivyo wanasema kuwa ikiwa kuna haja kama kwa mfano ardhi ina joto kali, miba na mfano wa hayo haina neno kuvaa viatu.

[1] Ahmad (5/83) na Abuu Daawuud (3230).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/200)
  • Imechapishwa: 25/08/2021