Ni ipi hukumu ya kuanza kuingia makaburini kwa mguu wa kushoto?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuanza kuingia makaburini kwa mguu wa kulia na kutoka na mguu wa kushoto?

Jibu: Hakuna Sunnah yoyote juu ya hilo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kujengea juu ya hilo mtu aingie vile itavyotokea. Ikitokea ameingia kwa mguu wa kulia, afanye hivo, na ikitokea ameingia kwa mguu wa kushoto, afanye hivo mpaka pale kutapopatikana dalili kutoka katika Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/167)
  • Imechapishwa: 25/08/2021