Ni ipi hukumu ya kutembea juu ya makaburi?

Swali: Ni ipi hukumu ya kutembea juu ya makaburi?

Jibu: Kutembea juu ya makaburi haijuzu kwa kuwa kuna kumtweza yule maiti. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuyatia chokaa makaburi, kujenga na kuyaandika juu yake. Amesema kuhusu kukaa juu yake:

“Mmoja wenu kukaa juu ya kaa likaunguza nguo zake na likaingia mpaka kwenye ngozi yake ni bora kwake kuliko kukaa juu ya kaburi.”[1]

[1] Muslim (971).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/202)
  • Imechapishwa: 25/08/2021