Ni ipi hukumu ya kuweka njia kwenye makaburi au kufanya ni sehemu ya kukaa?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuweka njia kwenye makaburi au kufanya ni sehemu ya kukaa?

Jibu: Haijuzu kuyafanya makaburi ya waislamu njia au sehemu ya kukaa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kukaa juu ya makaburi na kusema:

“Mmoja wenu kukaa juu ya kaa likaunguza nguo zake na likaingia mpaka kwenye ngozi yake ni bora kwake kuliko kukaa juu ya kaburi.”[1]

Ni wajibu vichochoro hivyo vilivyopo makaburini viondoshwe na makaburi ya waislamu yaheshimiwe.

[1] Muslim (971).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/203)
  • Imechapishwa: 25/08/2021