Ni ipi hukumu ya kufungua mafundo na kufunua uso wa maiti ndani ya kaburi?

Swali: Ni ipi hukumu ya kufungua mafundo na kufunua uso wa maiti pindi anapowekwa ndani ya kaburi?

Jibu: Kuhusu kufungua mafundo, imepokelewa ya kwamba ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mnapomuweka maiti ndani ya kaburi fungueni mafundo.”[1]

Kuhusu inapokuja katika kufunua uso wote wa maiti, ni jambo lisilo na asli. Kubwa lililopokelewa – kama itakuwa ni Swahiyh – ni maneno ya ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh):

“Nitapofariki na mkaniweka ndani ya kaburi, liacheni shavu langu liguse ardhi.”[2]

[1] Mtunzi wa “ar-Rawdhw al-Murbi´” amemnasibishia upokezi huu al-Athram na akasema kwenye taaliki: “Mfano wa haya yamepokelewa kutoka kwa Samurah.”

[2] Tazama ”al-Mughniy” (3/428) ya Ibn Qudaamah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/183)
  • Imechapishwa: 25/08/2021