Ni ipi hukumu ya kuweka jiwe katikati ya kaburi la mwanamke?

Swali: Baada ya kumaliza kumzika mwanamke mchimbaji wa kaburi anaweka jiwe lenye kuonekana katikati ya kaburi lake ili watu wote waweze kujua kuwa mwanamke ndiye ambaye yuko ndani ya kaburi. Wanatumia hoja kwamba kwa mfano ikitokea kulichimbua kutiliwe umuhimu kumsitiri viungo vyake vya siri. Je, kitendo hichi ni katika Sunnah?

Jibu: Sio katika Sunnah. Sunnah ni kulinyanyua kaburi kiasi cha shibri. Hakuna tofauti kati ya kaburi la mwanaume na la mwanamke. Lakini hata hivyo hakuna neno kuweka alama kwenye kaburi ili wale ndugu zake wanaotaka kumtembelea wamjue. Ama kutofautisha kwa kuweka jiwe hili ni jambo lisilokuwa na asli.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/174)
  • Imechapishwa: 25/08/2021