Ni ipi hukumu ya kupiga picha viumbe vyenye roho?

Swali: Ni ipi hukumu ya kupiga picha za jua kwa ajili ya haja au mapambo?

Jibu: Kupiga picha viumbe vyenye roho ni haramu isipokuwa kwa vile vinavyopelekea katika dharurah. Kwa mfano kuchukua picha kwa ajili ya uraia, pasipoti, kuwachukua picha majambazi kwa ajili ya kuwadhibiti na kuwajua na kuwashikia hatua pale watapokuwa wamefanya jarima na wanataka kukimbia na mfano wa picha kama hizi ambazo mtu hana budi kuwa nazo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/454)
  • Imechapishwa: 24/08/2020