Swali: Asiyehukumu kwa aliyoteremsha Allaah ni muislamu au ni kafiri aliyekufuru kufuru kubwa? Je, matendo yake yanakubaliwa?

Jibu: Amesema (Ta´ala):

“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.” (05:44)

“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio madhalimu.” (04:45)

“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio mafasiki.” (04:47)

Lakini hata hivyo akihalalisha hilo na akaonelea kuwa inajuzu, ni kufuru kubwa, dhuluma kubwa na ufusqa mkubwa wenye kumtoa katika Uislamu. Ama akifanya hayo kwa ajili ya rushwa au makusudio mengine na wakati huo huo anaamini kuwa ni haramu, ni mwenye kutenda dhambi. Anazingatiwa kuwa amefanya kufuru ndogo, dhulumu ndogo na ufusqa mdogo usiyomtoa katika Uislamu. Hivyo ndivyo walivyoweka wazi wanachuoni pindi walipozifasiri Aayah zilizotajwa.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/540)
  • Imechapishwa: 24/08/2020