Swali: Ni ipi hukumu ya mtu ambaye hatekelezi faradhi yoyote miongoni mwa faradhi zilizofaradhishwa kama swalah pamoja na kuwa yusalama na ni mwenye afya. Anawafanyia watu mambo mema na anajiepusha na shari na anasema “Allaah ni mwingi wa kusamehe na Mwenye kurehemu, mimi sifanyi shari na badala yake ni mtu napenda kufanya mambo ya kheri. Kuna watu ambao wanaswali na wanafanya mambo mazuri lakini kuna mambo wanayofanya kama uzinzi, ribaa na kunywa pombe pamoja na kuwa ni mwenye kuhifadhi swalah zote”. Ni ipi hukumu ya mtu kama huyu?

Jibu: Mosi ni kwamba kuacha swalah ni kufuru kubwa hata kama mtu hakukanusha uwajibu wake. Hii ndio kauli sahihi ya wanachuoni. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ahadi iliyopo baina yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo yule mwenye kuiacha amekufuru.”

Kuna Hadiyth nyinginezo zenye maana kama hiyo.

Pili kufanya zinaa ni moja katika madhambi makubwa. Kadhalika kutaamiliana na ribaa na kunywa pombe. Madhambi yote haya ni makubwa. Lakini mwenye kuyafanya hatoki katika Uislamu maadamu hayahalalishi. Lakini hata hivyo yuko katika khatari kubwa. Akifa ilihali ni mwenye kuendelea kuyafanya yuko chini ya matakwa ya Allaah; akitaka atamsamehe na akitaka atamuadhibu kiasi na dhambi madhambi yake. Pamoja na hivyo mafikio yake ya mwisho ni Peponi. Allaah (Ta´ala) amesema:

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa Amtakae.” (04:116)

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/507-508)
  • Imechapishwa: 24/08/2020