Swali: Kuna wanachuoni Uingereza wenye kuona inafaa kuchukua picha kwa wenye kuswali mkusanyiko na kuwachukua watoto picha wakati wanaposoma Qur-aan. Kwa kuwa picha hizi zinapoenezwa kwenye magazeti kuna uwezekano kwa wasiokuwa waislamu wakaathirika na wakapendezeshwa na kutaka kuujua Uislamu na waislamu.

Jibu: Kupiga picha viumbe walio na roho ni haramu, sawa picha ikiwa ni ya mtu au mnyama mwingine. Ni mamoja vilevile picha hiyo ikiwa ni ya mwenye kuswali, mwenye kusoma Qur-aan au wasiokuwa hao wawili. Kumethibiti maharamisho juu ya hayo katika Hadiyth ambazo ni Swahiyh. Haijuzu kueneza picha kwenye magazeti na barua hata kama zitakuwa ni za waislamu, wenye kutawadha au wenye kusoma Qur-aan kwa lengo la kueneza Uislamu na kuwapendezeshea wengine kuweza kuujua na kusilimu. Haijuzu kufanya mambo ya haramu kuwa ni njia ya kufikisha na kueneza Uislamu.

Njia za kufikisha zinazojuzu ni nyingi. Zisiachwe na kuchukuliwa nyinginezo ambazo Allaah ameharamisha.

Kuwepo kwa picha kwenye miji ya Kiislamu sio hoja ya kujuzu. Hayo ni maovu kutokana na dalili sahihi juu ya hayo. Kinachopaswa ni kukataza picha kwa kutendea kazi dalili.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/484-485)
  • Imechapishwa: 24/08/2020