Swali: Je, muumini atadumishwa Motoni ikiwa anamwamini Allaah na kadhalika? Ikiwa haswali anazingatiwa kuwa ni muumini?

Jibu: Muumini hatodumishwa Motoni hata kama atafanya dhambi kubwa mbali na kufuru. Akifa kabla ya kufanya tawbah atakuwa chini ya matakwa ya Allaah; akitaka atamuadhibu na mafikio yake ya mwisho itakuwa ni Peponi, na akitaka atamsamehe madhambi yake. Amesema (Ta´ala):

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa Amtakae.” (04:116)

Mwenye kuacha swalah ni kafiri aliyekufuru kufuru kubwa. Anastahiki kudumishwa Motoni milele kama makafiri wengine.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/489)
  • Imechapishwa: 24/08/2020