Swali: Je, ni sahihi kwa muislamu kuuza masanamu/mapicha na kufanya ndio bidhaa yake na akaishi kwayo?

Jibu: Haijuzu kwa muislamu kuuza masanamu au akatajirika kwayo. Kumethibiti Hadiyth ambazo ni Swahiyh zinazoharamisha kupiga picha viumbe wenye roho na kufanya kwazo masanamu na kubaki nazo. Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba kufanya biashara kwazo ni kuzieneza na ni kusaidia zikapigwa picha na zikawekwa kwenye manyumba, vitabu na kadhalika.

Ikishakuwa ni haramu basi kufanya biashara kwazo kwa kuzitengeneza na kuziuza ni haramu. Haijuzu kwa muislamu kuishi kwazo, ni mamoja kwa pato la chakula na mengineyo. Ikiwa ametumbukia katika hilo ni juu yake ajinasue nalo na atubu kwa Allaah (Ta´ala) huenda akamsamehe. Amesema (Ta´ala):

“Hakika Mimi bila shaka ni Mwingi wa kusamehe kwa anayetubia na akaamini na akatenda tendo njema kisha akaendelea kuongoka.” (20:82)

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (489/01)
  • Imechapishwa: 24/08/2020