Inajuzu kupiga picha za kumbukumbu ikiwa mtu hazitundiki ukutani?

Swali: Ni ipi hukumu ya picha zinazopatikana kwenye magazeti ya Kiislamu ambayo tunanunua? Ni ipi hukumu ya picha za kumbukumbu ambazo hazitundikwi ukutani? Je, inajuzu kubaki nazo na kuzihifadhi?

Jibu: Haijuzu kuhifadhi picha za kumbukumbu. Bali ni wajibu kuziharibu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh):

“Usiache picha (sanamu) isipokuwa umeiharibu, kaburi lililoinuka isipokuwa umelisawazisha.”

Ameipokea Imaam Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Kuhusu zinazopatikana kwenye kitabu au gazeti na wewe ni mwenye kuhitaji kukihifadhi, iharibu picha ijapokuwa uso wake na ubaki nacho kutokana na haja.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/483)
  • Imechapishwa: 24/08/2020