Kuyahifadhi magazeti ya kielimu yaliyo na picha

Swali: Unasemaje kuhusu kuhifadhi gazeti lililo na picha? Je, ni miongoni mwa picha zilizokatazwa?

Jibu: Kuhifadhi gazeti lililo na picha inajuzu ikiwa kulihifadhi ni kwa ajili ya ile elimu yenye manufaa iliyomo mle ndani. Linalotakikana kwa yule mwenye kulihifadhi aiharibu ile picha. Itakuwa haijuzu ikiwa kama kulihifadhi gazeti hilo ni kwa sababu ya hiyo picha.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/476)
  • Imechapishwa: 24/08/2020