Swali: Baadhi ya watu wanazungumza maneno ambayo yanaweza kuwa yanawapelekea katika kufuru au ufuska na huku anasema kuwa anafanya mzaha. Je, mzaha wake ni sahihi kumfanya asiwe na dhambi au sivyo?

Jibu: Mizaha [katika dini] imeharamishwa makatazo makubwa kutokana na ima kufuru inayopatikana ndani yake au dhambi kubwa. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَئِن سَأَلْتَهُمْ لَيَقُولُنَّ إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلْعَبُ ۚ قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ

“Ukiwauliza bila shaka watasema: “Hakika tulikuwa tunaporoja na tunacheza.” Sema: Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayah Zake na Mtume Wake?” Hivyo basi msitoe udhuru, mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.” (09:65-66)

Ni wajibu kutubu kwa kitendo hicho na kuomba msamaha. Huenda Allaah akamsamehe aliyefanya hivo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/32-33)
  • Imechapishwa: 24/08/2020