Faradhi za wudhuu’:

1 – Kuosha uso.

2 – Kuosha mikono mpaka kwenye visugudi.

3 – Kupangusa kichwa.

4 – Kuosha miguu mpaka kwenye vifundo. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ

“Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya swalah, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi na panguseni kwa [kupaka maji] vichwa vyenu na [osheni] miguu yenu hadi vifundoni.” (05:06)

Kuhusu kupangusa kichwa kunaingia pia masikio mawili. Kuhusu kuosha uso kunaingia pia kusukutua kinywa na kupalizia maji puani.

Katika wudhuu’ ni wajibu kuosha viungo hivi vinne. Mahala pa kuosha ni mara tatu. Mahala pa kupangusa ni mara moja.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/362-363)
  • Imechapishwa: 14/05/2023