27. Mtume akitahadharisha Bid´ah

Kuhusu Hadiyth za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zinazohusu mada hii, ni nyingi sana. Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule anayezipa mgongo Sunnah zangu basi si katika mimi.”[1]

´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu waliokuwa wananifuatawatanijia katika Hodhi. Pale tu nitakapowaona, basi watakatwa kutokamana nami. Nitasema: “Ee Mola wangu! Maswahabah zangu! Maswahabah zangu!” Nidipo kusemwe: “Hakika wewe hujui waliyoyazua kabla yako.”[2]

Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Hakika mazungumzo bora ni Kitabu cha Allaah na uongofu bora ni uongofu wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Uovu wa mambo ni yale yaliyozuliwa na kila Bid´ah ni upotevu.”[3]

Abu Hurayrah amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote anayelingania katika uongofu basi anapata ujira mfano wa yule mwenye kumfuata pasi na kupungua chochote katika ujira wao. Na yeyote anayelingania katika upotevu basi anapata dhambi mfano wa yule mwenye kumfuata pasi na kupungua chochote katika dhambi zao.”[4]

al-´Irbaadhw bin Saariyah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

al-´Irbaadhw:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitutolea mawaidha makali ambayo yalizitikisa nyoyo zetu na macho yetu yakatiririka machozi. Tukasema: “Ee Mtume wa Allaah! Ni kana kwamba ni mawaidha ya kutuaga; tuusie!” Akasema: “Ninakuusieni kumcha Allaah (´Azza wa Jall) na kusikiliza na kutii – yaani watawala – hata kama mtataliwa na mtumwa. Hakika yule atakayeishi katika nyinyi basi atakuja kuona tofauti nyingi. Hivyo basi, lazimianeni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu na wenye kuongoza baada yangu. Shikamaneni nazo kwelikweli na ziumeni kwa magego. Tahadharini na mambo yenye kuzuliwa, kwani hakika kila kilichozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”[5]

[1] al-Bukhaariy (5063) na Muslim (1052).

[2] al-Bukhaariy (6582) na Muslim (2304).

[3] Muslim (867), Ibn Maajah na wengineo.

[4] Muslim (2674).

[5] Abu Daawuud (4607), at-Tirmidhiy (2676) na Ibn Maajah (34). at-Tirmidhiy amesema:

“Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (2455).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 32-33
  • Imechapishwa: 14/05/2023