26. Tahadhari kwenda kombo na Sunnah

Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema tena:

فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

“Basi watahadhari wale wanaokwenda kinyume amri yake; isije kuwapata fitina au ikawapata adhabu iumizayo.”[1]

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:

“Ninashangazwa na watu wanaojua cheni ya wapokezi na usahihi wake lakini wanaamua kwenda katika maoni ya Sufyaan. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

“Basi watahadhari wale wanaokwenda kinyume amri yake; isije kuwapata fitina au ikawapata adhabu iumizayo.”[2][3]

Haafidhw Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) amesema:

“Bi maana watahadhari wale wanaoenda kinyume na amri ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), nayo ni ile njia, Sunnah na Shari´ah yake. Maneno na vitendo vyote vinatakiwa kupimwa kwa maneno na matendo yake. Yale yanayoafikiana na maneno na matendo yake, yatakubaliwa, na yale yanayoenda kinyume na maneno na matendo yake, ni yenye kurudishwa kwa mwenye nayo. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayefanya katika amri yetu hii kisichoafikiana na amri yetu kitarudishwa.”[4]

Kwa hivyo, atahadhari na aogope yule anayeenda kinyume na Shari´ah yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa ndani na kwa nje:

أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ

”… isije kuwapata fitina… ”

Bi maana katika nyoyo zao katika ukafiri, unafiki au Bid´ah.

أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

“…  au ikawapata adhabu iumizayo.”

Bi maana duniani kwa kuuliwa, kuadhibiwa, kufungwa na mfano wake.”[5]

[1] 24:63

[2] 24:63

[3] al-Ibaanah (1/260) ya Ibn Battwah.

[4] al-Bukhaariy (2697).

[5]Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/407).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 32
  • Imechapishwa: 14/05/2023