Swali: Mwanaume amemtaliki mke wake mara tatu ambapo baadaye akaolewa na mwanaume mwingine akamuoa kwa nia ya kumhalalishia yule mume wa kwanza, lakini pasi na mwanaume huyo kujua jambo hilo. Baadaye mwanaume huyo akamtaliki mwanamke huyo na akaolewa na yule mume wa kwanza na baadaye akaja kujua nia ya yule mume wa pili. Je, ndoa ni batili?

Jibu: Hapana, sio batili muda wa kuwa hakujua jambo hilo. Hata hivyo huyu mume wa pili anapata dhambi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (37)
  • Imechapishwa: 23/07/2023