Mke anashurutisha mume asiongeze mwanamke mwingine

Swali: Niliweka sharti wakati wa kuoa ya kuongeza mke nikisahilikiwa kufanya hivo…

Jibu: Huna haja ya kuweka sharti. Una haki ya kuongeza mke hata kama hukuweka sharti hiyo. Hakuna kinachokuzuia kuongeza mke. Hata hivyo mwanamke anayo haki ya kuweka sharti ya kutomuowea juu yake. Ukioa katika hali hiyo, anayo haki ya kufuta ndoa.

Swali: … hivi sasa nilipotaka kuongeza mke mwanamke akaomba kufuta ndoa. Je, anayo haki ya kufanya hivo?

Jibu: Hakuweka sharti hapo kabla. Kama alikuwekea sharti ya wewe kutoongeza mke, hapo ndipo anayo haki ya kufuta ndoa. Lakini kama hakukuwekea sharti, hana haki ya kuivunja ndoa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (37)
  • Imechapishwa: 23/07/2023