Swali: Ni ipi nasaha yako kwa yule ambaye ndoa inamzuia kutafuta elimu?
Jibu: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hakuweka ndoa ili ikuzuie na matendo mazuri, kutafuta elimu na kulingania katika dini ya Allaah. Baadhi ya watu wanapooa ndoa inawazuia na matendo mazuri mengi. Hii sio sababu ambayo Allaah ameweka ndoa kwa ajili yake. Ameiweka ili wewe na mke wako mzidishe kufanya matendo mazuri, kufanya Da´wah, du´aa, ´ibaadah na kutafuta elimu. Ndoa ni neema. Mtu anapopata neema mpya basi amshukuru Allaah kwayo. Lakini ikiwa unarudi nyuma kila wakati unapopata neema maana yake ni kwamba humshukuru. Allaah amesema:
لَئِن شَكَرْتُمْ لَأَزِيدَنَّكُمْ ۖ وَلَئِن كَفَرْتُمْ إِنَّ عَذَابِي لَشَدِيدٌ
“Mkishukuru, bila shaka Nitakuzidishieni na mkikufuru, basi hakika adhabu Yangu ni kali.” (14:07)
Izungumzishe nafsi yako ya kwamba kila wakati kunapokuja neema mpya basi majukumu na shukurani vinazidi. Hutakiwi kurudi nyuma.
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://olamayemen.com/index.php?article_id=2697
- Imechapishwa: 20/09/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Mwanafunzi na mke wake
Swali: Unamnasihi kitu gani mtu ambaye masomo yanamzuia kuoa? Vipi kijana atakusanya kati ya kuoa na masomo? Jibu: Ikiwa anaweza kusoma kwa muda wa mwaka, miwili, mitatu mpaka mine bila ya kuoa ili aweze kufikia elimu yenye manufaa ni bora. Ikiwa hawezi hilo na akaoa, achague na kuoa mwanamke mwema…
In "Elimu na masomo"
Amemuoa mwanamke ambaye mama hamtaki
Swali: Nimemuoa mwanamke ambaye mama yangu hayuko radhi naye, si kwa sababu ya dini yake, hampendi tu kwa sababu hakupendezwa naye. Ni zipi nasaha zako pamoja na kuzingatia kwamba tayari nimeshafunga naye ndoa? Allaah akujaze kheri. Jibu: Allaah akubarikini, juu yenu na akukusanyeni katika kheri. Hakuna yeyote anayestahiki kuingilia kati…
In "Kuwatendea wema wazazi"
01. Ifanyie kazi elimu yako
Tunamshukuru Allaah kwa yale aliyotupa ilhamu kwayo. Tunamuomba Allaah atuwafikishe kuyatendea kazi kwa vitendo yale tuliyoyajua. Kwani hakika kheri haifikiwi isipokuwa kwa tawfiyq na msaada Wake. Yule mwenye kuongozwa na Allaah, basi hakuna wa kumpotosha katika viumbe Wake. Swalah na amani zimwendee Muhammad, bwana wa viumbe wote, kwa ndugu zake…
In "Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal [elimu inapelekea matendo]"
