´Uthmaan. Yeye ni Abu ´Abdillaah Dhun-Nuurayn ´Uthmaan bin ´Affaan anayetokana na ukoo wa Banuu Umayyah bin ´Abdish-Shams bin ´Abd Manaaf. Alisilimu kabla ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuingia Daar-ul-Arqam. Alikuwa ni tajiri na mkarimu. Alichukua uongozi baada ya ´Umar bin al-Khattwaab kwa makubaliano ya watu wa mashauriano mpaka alipouliwa hali ya kuwa shahidi katika Dhul-Hijjah mwaka wa 35 H akiwa na miaka 90, haya ni moja ya maoni mbalimbali yaliyosemwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 141
  • Imechapishwa: 12/12/2022