´Umar. Yeye ni Abu Hafsw al-Faaruuq ´Umar bin al-Khattwaab anayetokana na ukoo wa Banuu ´Adiyy bin Ka´b bin Lu´ayy. Alisilimu katika mwaka wa sita baada ya takriban wanamme arobaini na wanawake kumi na moja. Waislamu wakafurahishwa naye na Uislamu Makkah ukapata nguvu baada yake. Abu Bakr alimteua kuongoza Ummah na akaongoza vyema mpaka alipouliwa hali ya kuwa shahidi katika Dhul-Hijjah mwaka wa 23 baada ya kuhajiri akiwa na miaka 63.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 141
  • Imechapishwa: 12/12/2022