Abu Bakr yeye ni as-Swiddiyq. Jina lake ni ´Abdullaah bin ´Uthmaan bin ´Aamir bin Banuu Taym bin Murrah bin Ka´b. Yeye ndiye mtumzima wa kwanza aliyemwamini Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yeye ndiye rafiki yake wakati wa Hijrah, naibu wake katika swalah na hajj na khaliyfah wake wa kwanza kwa Ummah wake. Wamesilimu kupitia mikono yake Maswahabah watano miongoni mwa wale waliobashiriwa Pepo; ´Uthmaan, az-Zubayr, Twalhah, ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf na Sa´d bin Abiy Waqqaas.

Alikufa Jumaadaa al-Aakhirah mwaka wa 13 H akiwa na umri wa miaka 63.

Watano hawa akiongezewa Abu Bakr, ´Aliy bin Abiy Twaalib na Zayd bin Haarithah wanakuwa wanane ambao wamewatangulia watu katika Uislamu. Haya yamesemwa na Ibn Ishaaq. Akimaanisha katika wanne baada ya Ujumbe.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 141
  • Imechapishwa: 12/12/2022