Swali: Nimemuoa mwanamke ambaye mama yangu hayuko radhi naye, si kwa sababu ya dini yake, hampendi tu kwa sababu hakupendezwa naye. Ni zipi nasaha zako pamoja na kuzingatia kwamba tayari nimeshafunga naye ndoa? Allaah akujaze kheri.
Jibu: Allaah akubarikini, juu yenu na akukusanyeni katika kheri.
Hakuna yeyote anayestahiki kuingilia kati suala la ndoa. Ni mamoja mama na baba. Isipokuwa tu pale watakapoona kitu kinachoitia kasoro dini. Kwa sababu suala hili linamuhusu mtu binafsi. Ni kama mfano wa chakula. Kwa mfano baba yako akikwambia usikaribie suala la kutafuta riziki, usiache. Jambo hili linamuhusu mtu mwenyewe. Mtu akitaka kumuoa mwanamke lakini mama yake akamwambia asimuoe, basi anatakiwa kumuuliza kama mwanamke huyo ana kasoro katika dini yake, heshima yake au ni kinyume na hivyo? Akisema kuwa hana kasoro lakini ni yeye tu hampendi, basi nasema: muoe na Allaah akubarikini, juu yenu na akukusanyeni katika kheri. Lakini baada ya hapo ni lazima kwake kujaribu kupatanisha kati ya mke wake na mama yake ili mambo yaweze kuwa mazuri na mtu, mama yake na mke wake waweze kukusanyika mahala pamoja. Ikiwa jambo hili haliwezekani na wakawa wanaishi katika nyumba moja – jambo ambalo linapelekea katika magomvi na mipasuko asubuhi na jioni – basi katika hali hii hakuna neno akatafuta nyumba nyingine pamoja na mke wake.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (66) http://binothaimeen.net/content/1475
- Imechapishwa: 19/01/2020
Swali: Nimemuoa mwanamke ambaye mama yangu hayuko radhi naye, si kwa sababu ya dini yake, hampendi tu kwa sababu hakupendezwa naye. Ni zipi nasaha zako pamoja na kuzingatia kwamba tayari nimeshafunga naye ndoa? Allaah akujaze kheri.
Jibu: Allaah akubarikini, juu yenu na akukusanyeni katika kheri.
Hakuna yeyote anayestahiki kuingilia kati suala la ndoa. Ni mamoja mama na baba. Isipokuwa tu pale watakapoona kitu kinachoitia kasoro dini. Kwa sababu suala hili linamuhusu mtu binafsi. Ni kama mfano wa chakula. Kwa mfano baba yako akikwambia usikaribie suala la kutafuta riziki, usiache. Jambo hili linamuhusu mtu mwenyewe. Mtu akitaka kumuoa mwanamke lakini mama yake akamwambia asimuoe, basi anatakiwa kumuuliza kama mwanamke huyo ana kasoro katika dini yake, heshima yake au ni kinyume na hivyo? Akisema kuwa hana kasoro lakini ni yeye tu hampendi, basi nasema: muoe na Allaah akubarikini, juu yenu na akukusanyeni katika kheri. Lakini baada ya hapo ni lazima kwake kujaribu kupatanisha kati ya mke wake na mama yake ili mambo yaweze kuwa mazuri na mtu, mama yake na mke wake waweze kukusanyika mahala pamoja. Ikiwa jambo hili haliwezekani na wakawa wanaishi katika nyumba moja – jambo ambalo linapelekea katika magomvi na mipasuko asubuhi na jioni – basi katika hali hii hakuna neno akatafuta nyumba nyingine pamoja na mke wake.
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (66) http://binothaimeen.net/content/1475
Imechapishwa: 19/01/2020
https://firqatunnajia.com/amemuoa-mwanamke-ambaye-mama-hamtaki/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)