Pepo iko juu ya ´Illiyyiyn:

كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْأَبْرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ

“Hashaa! Hakika kitabu cha watendao wema bila shaka kiko katika ‘Illiyyiyn.”[1]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kisa kinachotambulika cha al-Baraa´ bin ´Aazib kuhusu mtihani wa ndani ya kaburi:

“Aseme (´Azza wa Jall): “Kiandikeni kitabu cha mja wangu katika ´Illiyyiyn na mrudisheni ardhini.”

Moto uko chini ya vilivyo chini. Amesema (Ta´ala):

كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٍ

“Hashaa! Hakika kitabu cha watendao maovu bila shaka kimo katika Sijjiyn.”[2]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth ya al-Baraa´ bin ´Aazib iliyotangulia:

“Aseme (´Azza wa Jall): “Kiandikeni kitabu cha mja wangu katika Sijjiyn katika ardhi ya chini.”

[1] 83:18

[2] 83:07

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 132-133
  • Imechapishwa: 12/12/2022