Pepo na Moto havitomalizika. Amesema (Ta´ala):

جَزَاؤُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتُ عَدْنٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا

“Malipo yao yako kwa Mola wao; mabustani ya kudumu milele yapitayo chini yake mito hali ya kuwa ni wenye kudumu humo milele.”[1]

Aayah zinazosema kuwa Moto utakuwa milele ni nyingi. Kuhusu Moto yametajwa hayo maeneo matatu. Katika “an-Nisaa´”:

وَلَا لِيَهْدِيَهُمْ طَرِيقًا إِلَّا طَرِيقَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا

“… wala kuwaongoza njia; isipokuwa njia ya Jahannam wadumishwe humo milele.”[2]

Katika “al-Ahzaab”:

إِنَّ اللَّـهَ لَعَنَ الْكَافِرِينَ وَأَعَدَّ لَهُمْ سَعِيرًا  خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا 

“Hakika Allaah Amewalaani makafiri, na Amewaandalia moto uliowashwa vikali mno. Ni wenye kudumu humo abadi.”[3]

 Katika “al-Jinn:

وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَإِنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا

“Yeyote atakayemuasi Allaah na Mtume Wake, basi hakika atapata Moto wa Jahannam hali ya kudumu humo milele.”[4]

Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي عَذَابِ جَهَنَّمَ خَالِدُونَ لَا يُفَتَّرُ عَنْهُمْ وَهُمْ فِيهِ مُبْلِسُونَ

”Hakika wahalifu wamo kwenye adhabu ya [Moto wa] Jahannam watadumu milele. Hawatopumzishwa nayo nao humo watakata tamaa.”[5]

[1] 98:08

[2] 04:168-169

[3] 33:64-65

[4] 72:23

[5] 43:74-75

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 132
  • Imechapishwa: 12/12/2022