Namna ya kudhihirisha dini katika nchi ya makafiri

Swali: Kigezo cha kudhihirisha dini katika nchi ya makafiri ni kwamba akikutana na wakazi wake awaambie kuwa wao ni makafiri?

Jibu: Kudhihirisha dini ni kule yeye kuswali, kufunga, kulingania kwa Allaah, kuamrisha mema, kukemea maovu, kuwafunza watu kheri, kuwafunza watu kuabudiwa kwa Allaah pekee na kuwafunza watu shirki. Hailazimu awaambie watu kuwa ni makafiri. Muhimu alinganie kwa Allaah na inatosha. Huku ndio kudhihirisha dini.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22920/كيف-يكون-اظهار-الدين-في-بلاد-الكفار
  • Imechapishwa: 15/09/2023