Kushika uume kwa mkono wa kuume wakati wa kukojoa

Swali: Makatazo ya kugusa uume wakati wa kukojoa ni jambo maalum katika hali ya kukidhi haja ndogo?

Jibu: Imekatazwa kushika uume na mkono wa kulia. Aushike na mkono wa kushoto. Hata hivyo hakuna neno endapo atashika dhakari kwa mkono wa kuume katika hali isiyokuwa ya kukidhi haja ndogo. Kwani uume ni sehemu katika viungo vyake…

Swali: Vipi kuhusiana na makatazo katika hali isiyokuwa ya kukojoa?

Jibu: Hakuna makatazo katika hali isiyokuwa ya kukojoa. Hakuna makatazo. Makatazo ni yeye kuushika kwa mkono wake ilihali anakojoa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22917/حكم-مس-الذكر-باليمين-حال-البول-وغيره
  • Imechapishwa: 15/09/2023