Wote wamepokea kwamba:
“Faatwimah ni kipande changu. Mwenye kumuudhi basi kaniudhi. Mwenye kuniudhi amemuudhi Allaah.””
Hadiyth hii haikupokelewa kwa tamko hili. Bali imepokelewa kwa tamko lingine kama mfano wa Hadiyth ambayo ´Aliy alipoomba kumposa msichana wa Abu Jahl. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayh iwa sallam) akasimama na kusema:
“Banuu Haashim bin al-Mughiyrah wameniomba idhini kuwaozesha msichana wao kwa ´Aliy bin Abiy Twaalib. Mimi simpi idhini. Mimi simpi idhini. Mimi simpi idhini. Faatwimah ni kipande changu. Kinanikera mimi kile kinachomkera yeye na kinaniudhi mimi kile kinachomuudhi yeye. Hata hivyo mtoto wa Abu Twaalib amwache msichana wangu na amuoe msichana wao.”
Kwa hiyo sababu ya Hadiyth ni ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) kumposa msichana wa Abu Jahl. Hapana shaka yoyote kwamba sababu inaingia ndani ya tamko. Haijuzu kuondosha sababu yake kutoka ndani ya tamko.
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kinanikera mimi kile kinachomkera yeye na kinaniudhi mimi kile kinachomuudhi yeye.”
Ni jambo linalotambulika kwamba kumposa kwake msichana wa Abu Jahl ni jambo linamkera na kumuudhi. Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) linamkera hilo na kumuudhi. Ikiwa matishio haya yanamgusa mtendaji, basi mtu wa kwanza yanayomgusa ni ´Aliy bin Abiy Twaalib. Ikiwa matishio haya hayamgusi mtendaji, basi Abu Bakr ana haki zaidi ya kutoguswa nayo kuliko ´Aliy.
Kukisemwa kwamba ´Aliy alijirudi katika jambo hilo, basi hilo linapelekea kwamba hakukingwa na kukosea.
Ikiwa inawezekana mtu mwenye kumkera na kumuudhi Faatwimah anaweza kusamehewa kupitia tawbah, kadhalika inawezekana pia kupitia matendo mema yanayofuta makosa. Kwa sababu yaliyo makubwa kuliko dhambi hii yanafutwa na matendo mema, tawbah na majanga.
Kwani dhambi hii sio kufuru ambayo Allaah haisamehi isipokuwa kwa kutubia. Mambo yangelikuwa hivo basi ´Aliy – na ulinzi unaombwa kutoka kwa Allaah – angelikuwa ameritadi kutoka katika Uislamu tangu wakati wa uhai wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni jambo linalotambulika kwamba Allaah (Ta´ala) amemlinda ´Aliy na kitu kama hicho.
- Muhusika: Shaykh-ul-Islam Ahmad bin Taymiyyah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhaaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah (4/250-252)
- Imechapishwa: 14/12/2018
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
Faatwimah bint Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
Alikuwa ndiye bibi wa wanawake katika zama zake na sehemu ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alikuwa ni Umm Abiyhaa[1], msichana wa bwana wa viumbe, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Abul-Qaasim Muhammad bin ´Abdillaah bin ´Abdil-Muttwalib bin Haashim bin ´Abdil-Manaaf al-Qurashiyyah al-Haashimiyyah. Alizaliwa punde kdiogo kabla…
In "Wanawake"
Hili ni kwa Faatwimah peke yake
Swali: Wakati ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) alipotaka kuoa mwanamke mwingine juu ya bibi Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anhaa), Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia: “Mke ana haki zaidi ya kujivua katika ndoa.” Je, ni sahihi? Jibu: Si sahihi. Allaah (Ta´ala) amesema: فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم…
In "Uoaji wa wake wengi"
82. Machukizo ya Faatwimah
Miongoni mwa mambo bora kutaja hapa ni yale ambayo Umm Ja´far bint Muhammad bin Ja´far ya kwamba Faatwimah, msichana wake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), amesema: ”Ee Asmaa´! Hakika mimi nimechukizwa na yale yanayofanywa na wanawake wanapozikwa na nguo za kubana.” Asmaa´ akasema: ”Ee msichana wa Mtume wa Allaah…
In "4. Sharti ya nne ya jilbaab"