Swali: Allaah (Ta´ala) amesema:

عَالِمُ الْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَىٰ غَيْبِهِ أَحَدًا إِلَّا مَنِ ارْتَضَىٰ مِن رَّسُول

“Mjuzi wa ghaibu na wala hamdhihirishii yeyote ghaibu Yake. Isipokuwa yule Aliyemridhia miongoni mwa Mitume.” (72:26-27)

Je, walii katika Ummah wa Mtume ni mwenye kuwafuata kwa kujua mambo yaliyofichikana?

Jibu: Allaah (Subhaanah) amehukumu kuwa elimu ya mambo yaliyofichikana ni jambo maalum Kwake. Amesema:

قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ

“Sema: “Hakuna [yeyote yule miongoni mwa] waliomo katika mbingu na ardhi ajuaye ghaibu isipokuwa Allaah pekee.” (27:65)

Hakuvua katika hilo isipokuwa Aliyemridhia miononi mwa Mitume ndiye ambaye anamdhihirisha yale anayoyataka katika mambo yaliyofichikana. Allaah (Ta´ala) amesema:

عَالِمُ الْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَىٰ غَيْبِهِ أَحَدًا إِلَّا مَنِ ارْتَضَىٰ مِن رَّسُول

“Mjuzi wa ghaibu na wala hamdhihirishii yeyote ghaibu Yake. Isipokuwa yule aliyemridhia miongoni mwa Mitume.”

Mwenye kudai kuwa kuna mtu katika Ummah wa Manabii na wa Mitume ya kwamba anajua mambo yaliyofichikana ni mwongo. Mwenye kudai kuwepo yeyote katika mawalii na watu wema, ambao ni wafuasi wa Mitume katika imani na matendo, kwamba anajua mambo yaliyofichikana ni mwenye kusema uongo. Anakadhibisha yaliyoteremka katika Qur-aan na Hadiyth zilizothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zenye kufahamisha kuwa elimu ya mambo yenye kufichikana ni mambo maalum yenye kujua Allaah.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/120-121)
  • Imechapishwa: 24/08/2020