Qiyaamah kitasimama baada ya karne kumi na nne?

Swali: Nimesikia baadhi ya wanachuoni wetu wakisema kuwa katika Hadiyth kuna khabari yenye kusema “Qiyaamah kitakuwa baada ya karne kumi na nne na kitu”. Je, maelezo haya ni sahihi? Kwa vile kumeshapita karne kumi na nne na hakukupitika kitu.

Jibu: Hakuna anayejua kwa kulenga wakati wa Qiyaamah kitaposimama isipokuwa Allaah (Subhaanah). Hakuna katika Hadiyth Swahiyh yoyote chenye kutolea dalili juu ya usahihi wa yale aliyoyasema yule uliyemnasibishia maneno hayo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/120)
  • Imechapishwa: 24/08/2020