Swali: Nimesikia baadhi ya maneno ambayo yanakaririwa na baadhi ya watu. Nilikuwa nataka kujua ni upi msimamo wa Uislamu kwa maneno haya. Kwa mfano anapokufa mtu kuna wanaosema “Marehemu fulani” (فلان المرحوم) na ikiwa ni mtu mwenye cheo kikubwa wanasema “Fulani aliyesamehewa”. Je, watu hawa wamechungulia kwenye Ubao uliohifadhiwa na kujua kuwa fulani huyo amesamehewa na fulani mwingine amerehemewa? Imekuwa watu wanachukulia usahali kuhusiana na mambo haya. Amesema (Ta´ala) katika Qur-aan:

وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ

“Pindi Alipochukua Allaah fungamano la wale waliopewa Kitabu: Bila shaka mtakibainisha kwa watu na wala hamtokificha.” (03:187)

Naomba mnipe fatwa.

Jibu: Kuthibiti msamaha wa Allaah kwa mtu au kumrehemu (Subhaanah) baada ya kufa kwake ni katika mambo yaliyofichikana ambayo hayajui yeyote isipokuwa Allaah (Ta´ala). Isitoshe jengine, ni nani ambaye Allaah amemjuza hilo kupitia Malaika au Mitume Wake au Manabii Wake? Mtu kusema, mbali na hawa tuliyowataja, juu ya maiti kuwa Allaah amemsamehe au amemrehemu haijuzu. Isipokuwa tu yule ambaye kuna dalili juu yake kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vinginevyo itakuwa ni kuvurumisha bila ya kujua. Allaah (Ta´ala) amesema:

قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ

“Sema: “Hakuna [yeyote yule miongoni mwa] waliomo katika mbingu na ardhi ajuaye ghaibu isipokuwa Allaah Pekee.” (27:65)

عَالِمُ الْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَىٰ غَيْبِهِ أَحَدًا إِلَّا مَنِ ارْتَضَىٰ مِن رَّسُول

“Mjuzi wa ghaibu na wala hamdhihirishii yeyote ghaibu Yake. Isipokuwa yule Aliyemridhia miongoni mwa Mitume.” (72:26-27)

Hata hivyo kunatarajiwa kwa muislamu msamaha, rehema na kuingia Peponi. Hii ni fadhila na rehema kutoka kwa Allaah. Anatakiwa kuombewa msamaha na rehema badala ya kuelezea juu yake kwamba ni mrehemewa na amesamehewa.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com