Mtu anapokufa Malaika wanaomchunga hufa pamoja naye?

Swali: Tufutie juu ya Malaika wenye kuwakilishwa kwa mwanaadamu juu ya kuyadhibiti matendo yake katika kipindi cha uhai wake, nao ni “Raqiyb” na “´Atiyd”. Wakati mtu anakufa Malaika hawa na wao wanakufa pamoja naye? Ni wapi yanakuwa mafikio yao baada ya mtu kufariki?

Jibu: Hali za Malaika na kazi zao ni katika mambo yaliyofichikana. Hayajulikani isipokuwa kwa kuwepo dalili katika Qur-aan na Sunnah. Hakukuthibiti dalili juu ya kufa kwa Malaika mwenye kuandika mema na maovu wakati anapokufa yule ambaye wamewakilishwa juu yake ili kuandika mema na maovu yake kama ambavyo vilevile hakuna dalili juu ya kwamba wanaendelea kuishi na mafikio yao ya mwisho. Hilo linajua Allaah pekee. Hayo yaliyoulizwa sio katika mambo ambayo tumewajibishiwa kuyaamini na hayahusiani na matendo. Hivyo kuuliza juu ya mambo hayo ni kuingia katika kitu kisichokuhusu. Kwa hivyo tunamnasihi muulizaji asiingie katika kitu kisichomuhusu. Atumie bidii zake kuuliza juu ya mambo ambayo yatamletea yeye na waislamu manufaa katika dini na dunia yao.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/124)
  • Imechapishwa: 24/08/2020