Wasiwasi wa kwamba mtu anajionyesha katika vitendo vyake

Swali: Mimi naswali, nafunga, nasoma Qur-aan na napambana ili niweze kutekeleza maamrisho ya Qur-aan na Sunnah. Lakini hata hivyo napata hisia za kwamba sifanyi haya isipokuwa ili kusemwe “huyu ni mtu wa dini”. Hisia hizi zinaweza kunifanya kuacha kufanya mambo fulani kwa kuchelea. Vipi nitajinasua na hili?

Jibu: Ni juu yako kutekeleza maamrisho ya Uislamu kwa kujisalimisha na maamrisho ya Allaah na kutaka thawabu zake. Puuzia wasiwasi unaokujia juu ya kwamba matendo yako haya ni kujionyesha. Pambana na wasiwasi huo kiasi na utakavyoweza.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/133)
  • Imechapishwa: 24/08/2020