Kijana wa dini anahisi yuko London anafanya machafu

Swali: Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 19. Namshukuru Allaah kuona naswali swalah tano zote msikitini kwa mkusanyiko ikiwa ni pamoja na Fajr. Baadhi ya nyakati naadhini msikitini na nimehifadhi karibu juzu sita. Lakini hata hivyo kuna kitu kinanipa dhiki sana, nacho ni kwamba pindi nakuwa nimekaa peke yangu au nimelala najiwa na fikra na kuwaza – na naomba kinga kwa Allaah – ya kwamba nimesafiri kwenda London, nimefanya zinaa na kukutana na wasichana waovu. Je, napata dhambi kwa hilo kwa kuzingatia ya kwamba hili haliniathiri. Hufanya punyeto ingawa ni mara chache sana. Nachelea ikanigusa Hadiyth yenye maana:

“Yule ambaye swalah yake haimzuii na machafu na maovu basi Allaah atamzidishia umbali.”

Jibu: Mosi wasiwasi na yale yanayoelezwa na moyo muislamu haadhibiwi kwayo. Imethibiti kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Ta´ala) ameusamehe Ummah wangu kwa yale yanayoelezwa na nafsi zao midhali hawajayatamka.”

Pili kujitoa manii kwa mkono kitu kinachoitwa “punyeto” ni haramu.

Tatu Hadiyth uliyotaja ni dhaifu. Lakini maana yake inajulikana kwa kikosi katika Maswahabah na Taabi´uun (Radhiya Allaahu ´anhum).

Tunataraji kuwa wasiwasi hautokushughulisha maadamu umejiepusha na maasi.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/133)
  • Imechapishwa: 24/08/2020