Mwanaume kumtazama mposwaji na kinyume chake

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mmoja wenu akimposa mwanamke, akiweza kumwangalia yale yatayomvutia kumuoa, basi na afanye hivo.”[1]

Ni yepi ambayo inafaa kwa mposaji kuyatazama kwa mposwaji?

Jibu: Atazame uso wake na mikono yake. Hayo ndio ambayo yanafaa kwake.

Swali: Je, mwanamke anayo haki ya kuomba kumtazama mposaji?

Jibu: Ndio. Anayo haki ya kuomba kumtazama kama anamfaa au hamfai.

[1] Abu Daawuud (2082). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy i ”al-Irwaa’” (1791).Tazama ”as-Swahiyhah” (99).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (45)
  • Imechapishwa: 20/07/2024