Mwanamme anayesikia adhaana na asiitikie

Swali: Mwenye kusikia wito na asiuitikie, basi hana swalah isipokuwa kwa udhuru.

Jibu: Kunakusudiwa swalah timilifu na iliyokamilika. Vinginevyo swalah yake ni sahihi na si batili. Zipo dalili nyenginezo ikiwa ni pamoja na ile ambayo alitamani kuzichoma nyumba zao na wala hakuwaamrisha kuzilipa. Kwa maana nyingine hakuwaamrisha kuzirudia. Yule ambaye alikuja na akaswali pamoja naye Fajr Minaa hakumwamrisha kuirudia. Alisema:

“Anaposwali mmoja wenu nyumbani kwake kisha akakutana na swalah basi aswali.”

Alimwambia Abu Dharr:

“Unapokutana na swalah, basi swali. Hakika kwako inakuwa ni kujitolea.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22502/حكم-من-سمع-النداء-للصلاة-فلم-يجبه
  • Imechapishwa: 30/06/2023