Swali: Je, inajuzu kwa mwanaume kumpeleka mke wa ndugu yake kwao ndani ya mji au ndani ya nchi, hali ya kuwa mke wake na watoto wake wadogo wako pamoja naye katika gari na mke wa ndugu yake ni dada wa mke wake?

Jibu: Hili ni kanuni watu wengi wanauliza: hapana, hapana, haifai aende naye, si pamoja na ndugu wa mume wake, wala pamoja na mke, wala pamoja na dereva. Ni lazima awepo wa tatu au wa nne kwa kujiepusha na fitina. Sababu nyingine hili lina aina ya kuwa faragha mwanaume na mwanamke. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Asikae mwanaume faragha na mwanamke isipokuwa shaytwaan anakuwa wa tatu wao.”

“Asikae mwanaume faragha na mwanamke isipokuwa pamoja naye yupo Mahram.”

Ikiwa yuko peke yake kuna khatari ya kuwepo baina yake na yeye jambo fulani; ahadi au maneno. Shaytwaan anaweza kuwatia wasiwasi baina yao. Kwa hiyo inafaa awepo pamoja nao wa tatu: mama yake, dada yake, ndugu yake au fulani miongoni mwa wale ambao hakuna shaka kwao. Kwa maana njia ambayo haina shaka ili iwe mbali zaidi na shaytwaan. Hata kama ni ndani ya mji, shuleni au katika matembezi ya baadhi ya jamaa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3491/حكم-سفر-المراة-مع-اخي-زوجها-وزوج-اختها
  • Imechapishwa: 04/09/2026