111. Wakeze Mtume (صلى الله عليه وسلم)

Wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao alitengana nao kwa kufa:

1 – Khadiyjah bint Khuwaylid. Yeye ndiye mama wa watoto wake tukimwondoa Ibraahiym. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuoa baada ya kuolewa na waume wawili; ´Atiyq bin ´Aabid na wa pili ni Abu Haalah at-Tamiymiy. Hakumuolea (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu yake mpaka alipofariki mwaka wa 10 baada ya kutumilizwa kabla ya kupandishwa juu mbinguni.

2 – ´Aaishah bint Abiy Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Alimuona (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usingizini[1] mara mbili au mara tatu na akaambiwa kuwa huyo ni mke wako. Akamuoa Makkah akiwa na miaka sita na akamwingilia al-Madiynah akiwa na miaka tisa. Alifariki mwaka wa 58 baada ya kuhajiri.

3 – Sawdah bint Zam´ah al-´Aamiriyyah. Alimuoa baada ya mume muislamu ambaye Sukraan bin ´Amr ambaye ni kaka yake Suhayl bin ´Amr. Alifariki mwishoni mwa uongozi wa ´Umar. Kuna maoni vilevile yanayosema kuwa ilikuwa katika mwaka wa 54 baada ya kuhajiri.

4 – Hafswah bint ´Umar bin al-Khattwaab. Alimuoa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)  baada ya mume muislamu ambaye ni Khunays bin Hudhaafah ambaye aliuliwa katika Uhud na akafariki mwaka wa 41 baada ya kuhajiri.

5 – Zaynab bint Khuzaymah al-Hilaaliyyah. Yeye ni mama wa masikini. Alimuoa baada ya mume wake ´Abdullaah bin Jahsh kufa shahidi katika Uhud na akafariki mwaka wa 04 muda mfupi baada ya ndoa ya kwanza.

6 – Umm Salamah Hind bint Abiy Umayyah al-Makhzuumiyyah. Alimuoa baada ya kufariki kwa mume wake Abu Salamah ´Abdullaah bin ´Abd-il-Asad kutokana na jeraha lililompata katika Uhud na akafariki mwaka wa 61 baada ya kuhajiri.

7 – Zaynab bint Jahsh al-Asadiyyah ambaye ni msichana wa shangazi yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alimuoa mwaka wa 05 baada ya mtumwa wake Zayd bin al-Haarithah aliyemwacha huru na akafariki mwaka wa 20 baada ya kuhajiri.

8 – Juwayriyyah bint al-Haarith al-Khuza´iyyah. Alimuoa baada ya mume wake Musaafiy´ bin Swafwaan. Kuna maoni mengine yanasema ni Maalik bin Swafwaan mwaka wa 06 baada ya kuhajiri na akafariki mwaka wa 56 baada ya kuhajiri.

9 – Umm Habiybah Ramlah bint Abiy Sufyaan. Alimuoa baada ya mume aliyesilimu kisha akawa mkristo. Ni ´Ubaydullaah bin Jahsh. Alifariki al-Madiynah katika uongozi wa kaka yake mwaka wa 44 baada ya kuhajiri.

10 – Swafiyyah bint Hayy bin Akhtwab ambaye anatokana na Banuu an-Nadhwiyr ambaye ni katika kizazi cha Haaruun bin ´Imraan (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alimwacha huru na akafanya kumwacha kwake huru ndio mahari yake baada ya waume zake wawili; wa kwanza alikuwa ni Sallaam bin Mushkim na wa pili ni Kinaanah bin Abiy al-Haqiyq baada ya kufungua mji wa Khaybar mwaka wa 06 baada ya kuhajiri na akafa mwaka wa 50 baada ya kuhajiri.

11 – Maymuunah bint al-Haarith al-Hilaaliyyah. Alimuoa mwaka wa 07 baada ya kuhajiri katika ´Umrah ya kulipa baada ya waume wawili; wa kwanza ni Ibn ´Abd Yaalayl na wa pili ni Abu Raham bin ´Abdil-´Uzza. Alimwingilia huko Sarif na akafa mwaka wa 51 baada ya kuhajiri.

Hawa ndio wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao alitengana nao kwa kufariki. Wakeze wawili walikufa kabla yake; Khadiyjah na Zaynab bint Khuzaymah. Wakeze wengine tisa alifariki baada yake akawaacha hai.

Wamebakia wanawake wawili ambao hakuwaingilia na wala hazithubutu kwao hukumu na ubora zinazothubutu kwa wale wengine waliotangulia. Nao ni wafuatao:

1 – Asmaa´ bint an-Nu´maan al-Kindiyyah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuoa kisha akamwacha. Kuna maoni mbalimbali kuhusu sababu ya kumwacha kwake. Ibn Ishaaq amesema kuwa alipata kiunoni mwake weupe ambapo akamwacha kisha baada yake Mtume al-Muhaajir bin Abiy Umayyah akamuoa.

2 – Umaymah bint an-Nu´maan bin Sharaahiyl al-Jawniyyah. Naye ndiye ambaye alimwomba Allaah amlinde kutokamana naye ambapo akamwacha[2]. Allaah ndiye mjuzi zaidi.

[1] al-Bukhaariy (3895) na Muslim (2438, 79).

[2] Rerejea ”Talkhiys-ul-Habiyr” (02/132-133) ya Ibn Hajar.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 153-154
  • Imechapishwa: 17/12/2022