Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

Mauti yataletwa katika sura ya kondoo mweupe. Atachinjwa kati ya Pepo na Moto. Kisha kutasemwa: “Enyi watu wa Peponi! Mtadumu na wala hakuna kufa tena! Enyi watu wa Motoni! Mtadumu na wala hakuna kufa tena!”[1]

MAELEZO

Kifo ni kuondoka kwa uhai. Kila nafsi itaonja kifo. Ni jambo la kimaana lisilohisiwa kwa kuonekana. Lakini Allaah (Ta´ala) atayafanya ni kitu chenye kuonekana na kilicho na kiwiliwili. Yatachinjwa kati ya Pepo na Moto kutokana na Hadiyth ya Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mauti yataletwa katika sura ya kondoo mweupe. Ataita kwa sauti Mwenye kuita kwa sauti: “Enyi watu wa Peponi! Watainua shingo zao na kuangalia. Kisha aseme: “Je, mnajua kitu hichi?” Waseme: “Ndio, hiki ni kifo. Wote waliyaona.” Kisha aite kwa sauti: “Enyi watu wa Motoni! Watainua shingo zao na kuangalia. Kisha aseme: “Je, mnajua kitu hichi?” Waseme: “Ndio, hiki ni kifo. Wote waliyaona. Yatachinjwa. Halafu aseme: “Enyi watu wa Peponi! Mtadumu na wala hakuna kufa tena! Enyi watu wa Motoni! Mtadumu na wala hakuna kufa tena!” Kisha akasoma:

وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ الْحَسْرَةِ إِذْ قُضِيَ الْأَمْرُ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ وَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ

“Waonye Siku ya majuto itakapohukumiwa amri na hali wao wamo katika ghafla, wala hawaamini.”[2]

Ameipokea al-Bukhaariy alipokuwa anafasiri Aayah hii[3] na amepokea mfano wake alipokuwa akielezea sifa ya Pepo na Moto kupitia kwa Ibn ´Umar ambaye amesimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[4].

[1] al-Bukhaariy (4730) na Muslim (2849).

[2] 19:39

[3] al-Bukhaariy (4730).

[4] al-Bukhaariy (6548).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 133-134
  • Imechapishwa: 12/12/2022