Swali: Je, inajuzu kufanya Twawaaf kwa niaba ya maiti?

Jibu: Haina asili, hapana. Ni kama ilivyo swalah kwa niaba ya maiti. Lililo dhahiri ni kwamba halifai. Kuhusu ´Umrah kamili na Hajj kamili, hapana ubaya.

Swali: Vipi kumfanyia aliye hai?

Jibu: Aliye hai pia hivyo hivyo. Wamelitaja baadhi ya wanazuoni, lakini halina dalili. Twawaaf ni katika aina ya swalah. Kwa hivyo haitofanyiwa Twawaaf isipokuwa kwa dalili na haiswaliwi isipokuwa kwa dalili. Hivyo hafanyiwi Twawaaf wala haswaliwi mtu kwa niaba ya mwingine. Lakini ikiwa atafanyiwa ´Umrah kamili au Hajj kamili – naye ni maiti au ni asiyeweza kama mzee mkongwe au kikongwe – basi hilo halina ubaya.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3511/حكم-الطواف-عن-الميت-او-الحي
  • Imechapishwa: 04/09/2026