Mume analala chumba kingine kwa kukimbia kero za watoto

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kulala katika chumba kingine pasipo mume wake kutokana na watoto wake wadogo kwa sifa ya kila siku kwa hoja eti ya kazi na mwanamke anakereka na tabia hiyo?

Jibu: Muhimu ni kuwa analala katika hiyo nyumba ambayo yuko mwanamke huyo. Si lazima alale naye kwenye kitanda kimoja. Alale katika nyumba ya mwanamke huyo na awe karibu naye. Hiki ndio kinachotakikana. Lakini akilala naye katika kitanda kimoja ndio bora zaidi. Hata hivyo sio lazima.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 13/04/2023