Muislamu mtenda dhambi na fasiki ni bora kuliko kafiri

Swali: Wako wanaosema kuwa kueshi katika miji ya makafiri ndio bora kuliko kueshi katika miji ya waislamu kwa sababu miji ya makafiri wako makafiri peke yake lakini hakuna wanafiki.

Jibu: Tunamuomba Allaah usalama. Huyu anawasifu makafiri na kuwatukana waislamu. Waislamu, hata kama watakuwa na maasi na mambo mengine, ni wabora kuliko makafiri. Muislamu mtenda dhambi na fasiki ni bora kuliko kafiri. Kafiri hakuna kheri kwake kabisa. Shari yake ni tupu. Lakini huyu yuko na kheri na shari. Kwa ajili hiyo ni mbora kuliko kafiri. Huyu kwa maana nyingine anapinga kuhajiri. Allaah amewajibisha kuhama kutoka katika nchi za makafiri na kwenda katika miji ya waislamu. Huyu anapinga na kuwaambia watu wasihajiri kwa sababu eti nchi za makafiri ni nzuri zaidi kuliko miji ya waislamu. Huu ni upotofu. Amesema (Ta´ala):

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُؤْمِنُونَ بِالْجِبْتِ وَالطَّاغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا هَـٰؤُلَاءِ أَهْدَىٰ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا سَبِيلًا أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ ۖ وَمَن يَلْعَنِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ نَصِيرًا

“Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaamini masanamu na ukafiri na wanasema juu ya wale waliokufuru: wameongoka zaidi katika njia kuliko wale walioamini – hao ndio wale Allaah aliowalaani; na ambaye Allaah amemlaani basi hutamkuta kuwa na mtu wa kumnusuru.”[1]

[1] 04:50-51

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 27/03/2023