Swali: Baadhi ya wanafunzi wanawakataza watu kuwazungumzia wanaoenda kinyume na mfumo wa Salaf kwa sababu ni waislamu. Wanaotakiwa kuzungumziwa ni makafiri peke yao na kutahadharisha kutokana nao.

Jibu: Hawa ndio wana haki zaidi ya kuzungumziwa. Kwa sababu ni waislamu. Waislamu ndio wana haki zaidi kunasihiwa:

وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ

“Na onya jamaa zako wa karibu.” (26:214)

Wao ndio wana haki zaidi kunasihiwa, kuwaidhishwa na kuzinduliwa makosa. Wao ndio wana haki zaidi. Inatakiwa kuanza na wao kwanza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 27/03/2023